WAJUMBE wa chama tawala cha National Resistance Movement nchini Uganda wamepitisha mapendekezo ya kubadili katiba yao na hivyo kumfanya katibu mkuu Amama Mbabazi kuwa hana kazi.
Mbabazi anafikiriwa kuwa ana nia ya kuwania Urais mwaka wa 2016 nchini Uganda dhidi ya rais wa sasa Yoweri Museveni.
Moja wa wajumbe walioshiriki ni mbunge wa Soroti mjini Mashariki mwa Uganda na pia Makamu Mwenyekiti wa wa NRM kanda ya mashariki Mike Mukula ambaye anasema katika marekebisho ya katiba ya chama hicho, sasa katibu mkuu wa chama atakuwa akiteuliwa na mwenyekiti.