Mbunge ajiuzulu baada ya kuiba mkate

Mbunge ajiuzulu baada ya kuiba mkate

Like
744
0
Friday, 15 February 2019
Global News

Mbunge mmoja nchini Slovenia amejiuzulu baada ya kuiba mkate maarufu ”sandwich” katika duka moja kwa madai kuwa wahudumu wa sehemu hiyo walimpuuzia.

Darij Krajcic ameviambia vyombo vya habari vya ndani kuwa alipuuzwa na wafanyakazi wa duka hilo na walikua wakiendelea na shuguli zao.

Hakujilakana kama ameiba lakini baadae baadhi ya wanachama walisisitiza arudi kulipa pesa ya mkate huo.

Krajcic ameomba msamaha na kusema kuwa anajutia kitendo alichokifanya.

Suala lake la kuiba lilisambaa baada ya kuwaambia wabunge wengine wakati wa mkutano wa kamati siku ya Jumatano.

”Nilisimama pale kwa dakika tatu, kabla wanihudumie,” mbunge huyo mwenye miaka 54 alisimulia katika kituo cha runinga cha mtu binafsi.

Wafanyakazi watatu wa duka hilo hawakugundua kama yupo baada ya kuwa walikua na mazungumzo baina yao hali iliyosabisha profesa huyo wa zamani kujaribu bahati yake.

”Hakuna mtu yoyote aliyepiga kelele, wala kunifuata.”

Wabunge wenzake walicheka baada ya kusikia kisa hicho.

Lakini siku ya Alhamisi spika wa bunge hilo Brane Golubovic, alikemea vikali kitendo cha mbunge kuiba, na kusema kuwa ni kitendo kisichokubalika.

”Amechukua hatua za kuwajibika na kujiuzulu yeye mwenyewe,” Golubovic aliviambia vyombo vya habari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *