MBUNGE WA JIMBO LA UKONGA EUGEN MWAIPOSA AWEKWA KIKAANGONI NA WANANCHI

MBUNGE WA JIMBO LA UKONGA EUGEN MWAIPOSA AWEKWA KIKAANGONI NA WANANCHI

Like
459
0
Thursday, 30 October 2014
Local News

WAKAZI wa kata ya kivule manispaa ya ilala jimbo la ukonga wamemlalamikia Mbunge wa jimbo hilo EUGEN MWAIPOSA kutotatua kero zinazokwamisha shughuli za kimaendeleo katika kata yao.

Wakazi hao wamezitaja kero hizo kuwa ni pamoja na kutogawanywa kwa kata hiyo yenye zaidi ya watu elfu 72 hali inayochangia kuwepo kwa migogoro ya Ardhi,

Akitoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya kutogawanywa kwa kata hiyo katika mitaa Mh.MWAIPOSA amesema swala hilo limeshafikishwa katika ofisi husika na zipo katika hatua za utekelezwaji hivyo itakapo kamilika ombi lao litatekelezwa.

Comments are closed.