MCHAKA MCHAKA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

MCHAKA MCHAKA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Like
233
0
Friday, 09 October 2015
Local News

ZIKIWA zimesalia siku chache kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, wagombea mbalimbali wemeendelea kutoa ahadi zao kwa wananchi huku wengi wakisisitiza kufanyia mabadiliko mambo mbalimbali ikiwemo, elimu, viwanda na suala zima la kukuza uchumi.

Mgombea ubunge wilaya ya kilolo  kupitia chama cha mapinduzi -CCM ameahidi kufanya mabadiliko katika tarafa tatu  wilayani humo na  kuleta maendeleo ya kasi.

Kwa uapnde wake, Mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA, mchungaji Peter Msigwa amewaahidi wananchi wa jimbo hilo kukuza uchumi na kwamba ataboresha sekta ya michezo, kupanua kiwanja cha ndege pamoja na kuweka taa za sola katika barabara .

Comments are closed.