MCHAKATO WA KUMALIZA KERO YA MIUNDOMBINU WAANZA KUFANYIWA KAZI TANDIKA

MCHAKATO WA KUMALIZA KERO YA MIUNDOMBINU WAANZA KUFANYIWA KAZI TANDIKA

Like
362
0
Wednesday, 16 March 2016
Local News

DIWANI wa kata ya Tandika Ramadhani Litumangiza amesema kuwa mchakato wa kuimaliza kero kubwa ya miundombinu ya barabara za ndani ya mtaa huo ambazo zimekuwa na mashimo na kutopitika kipindi cha mvua umekamilika na kuanza kufanyiwa kazi hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Tandika jijini Dar es salaam, Diwani Ramadhani amesema kuwa kumekuwa na kero hiyo ambapo kipindi cha mvua maji hujaa kwenye madimbwi yaliyopo barabarani na kuingia kwenye nyumba za watu.

Ameongeza kuwa tayari amefanikiwa kupata mradi wa ujenzi wa mifereji ya maji katika kata hiyo utakaogharimu shilingi milioni 50 na kuwa jitihada zaidi za kuhakikisha kero za msingi zinatatuliwa ikiwemo sekta ya elimu na afya .

Comments are closed.