MCHAKATO WA UHAMASISHAJI WA KATIBA MPYA KUANZA IVORY COAST

MCHAKATO WA UHAMASISHAJI WA KATIBA MPYA KUANZA IVORY COAST

Like
255
0
Monday, 24 October 2016
Slider

Waungaji mkono mswada mpya wa katiba wenye utata, wamezindua kampeini ya kuwapata wapigaji kura wengi zaidi, ili kubioresha katika kura ya maoni, itakayopigwa mnamo Octoba 30 mwaka huu, licha ya wito wa upinzani wa kuipinga.

Kambi ya Ndio inayoongozwa na serikali ya Rais Alassane Ouattara, inachukulia kura hiyo ya maoni kama fursa ya kufungua ukurasa mpya wa kutanzua mzozo wa muda mrefu nchini Ivory Coast, na kutanzua maswala yenye utata ya ni nani anayefaa kuwania kiti cha Urais.

Baadhi ya vipengee katika rasimu ya katiba mpya ni kuondoa kifungu kinachosema wazazi wote wawili wa muwaniaji kiti cha Urais, wanafaa kuwa wazaliwa wa Ivory Coast.

Awali, kifungu hicho kilimzuia Bw Ouattara kuwania kiti cha Urais.

Katiba mpya pia inaweka umri wa juu zaidi kwa muwaniaji kiti cha Urais, kuwa chini ya miaka 75, jambo linalosababisha tetezi kubwa ndani ya vyama vya upinzani kuwa Bw Ouattara, 74, anapania kutafuta muhula wa tatu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Akipuuzilia mbali ujumbe wa serikali kuwa katiba mpya itaboresha amani na kukuza amani na maadili katika taifa lililosambaratishwa na mizozo, mwanasayansi wa kisiasa Jean Alabro, ananukuliwa na shirika la habari la AFP: Sawa tu na katiba ya sasa inavyompinga Bw Ouattara, hii mpya inampendelea Ouattara na kambi yake.”

Rasimu hiyo ya katiba mpya pia, inaendekeza kubuniwa kwa cheo cha naibu wa Rais, hatua ambayo wapinzani wa Bw Ouattara wanasema kwamba inatoa nafasi kwa kumuandaa mtu kama mrithi wake anapoondoka madarakani.

Juma lililopita, walinda usalama walivunja maandamano ya wapinzani dhidi ya katiba hiyo mpya mjini Abidjan.

Katiba hiyo mpya inatarajiwa kuidhinishwa kupitia kura ya maoni, huku wafuasi wa Bw Ouattara, watakapojitokea kupiga kura tofauti na wafuasi wa upinzani, ambao wameamua kususia shughuli hiyo, baada ya wito kutolewa na vyama vyao.

Comments are closed.