Mchekeshaji Bill Cosby amehukumiwa hadi miaka 10 jela kwa unyanyasaji wa kingono

Mchekeshaji Bill Cosby amehukumiwa hadi miaka 10 jela kwa unyanyasaji wa kingono

Like
455
0
Wednesday, 26 September 2018
Global News

Jaji huko Pennsylvania amemhukumu jela mchekeshaji Bill Cosby kifungo cha kati ya miaka 3 na 10 kwa unyanyasaji wa kingono.

Cosby, 81, pia aliorodheshwa kuwa mtu mwenye tabia unyanyasaji wa kingono ikimaanisha kuwa ni lazima ashauiriwa katika maisha yake yote na kuwekwa kwenye daftari ya wanyanyasaji wa kingono.

Mchekeshaji huyo huyo alikataa kusema lolote hata baada ya kupeea fursa ya kufanya hivyo.

Wakati wa kusikilizwa tena kwa kesi hiyo mwezi April, Cosby alikutwa na hatia ya makosa matatu ya unyanyasaji wa kingono kwa kumlewesha na kumnyanyasa kingono Andrea Constand mwaka 2004.

Ombi la Cosby la kutaka kuachiliwa kwa dhamana akisubiri rufaa lilikataliwa.

Mchekeshaji huyo alitapa umaarufu miaka ya 1980 wakati alishiriki katika kipindi cha televisheni kuhusu familia ya Kimarekani yenye asili ya Afrika iliyokuw ikiishi Brooklyn, New York.

Alipata umaarufu sana hadi kufikia kupewa jina “America’s Dad”.

Mwezi Juni mwaka 2017 Canstand alieleza jisni Cosby ambaye alimuona kama mshauri wake akimpa vidonge ambavyo vilemlewesha hadi asiweze kuzuia unyanyasaji uliokuwa ukiendelea

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *