MCHINA AKIRI KUIBA SIRI ZA MAREKANI

MCHINA AKIRI KUIBA SIRI ZA MAREKANI

Like
280
0
Thursday, 24 March 2016
Global News

MWANAMUME mmoja kutoka Uchina amekiri kuhusika katika njama ya kuiba siri kuu kuhusu mifumo ya kijeshi ya Marekani.

Su Bin anaaminika kuwa kwenye kundi la watu ambao wamekuwa wakiiba habari kuhusu ndege za kivita, ndege za kubeba mizigo na silaha.

Bw Su, mwenye umri wa miaka 50, alikiri kufanya kazi na watu wawili kutoka Uchina kati ya Oktoba 2008 na Machi 2014 kudukua mifumo ya kompyuta ya Marekani, ikiwemo kampuni ya Boeing inayotumiwa na jeshi la Marekani kuunda ndege zake.

Comments are closed.