MELI ILIYOBEBA MADINI YA URANI YANG’OA NANGA IRAN

MELI ILIYOBEBA MADINI YA URANI YANG’OA NANGA IRAN

Like
258
0
Tuesday, 29 December 2015
Global News

MELI iliyobeba kilo 11,000 za madini ya Urani ambayo yamerutubishwa kwa kiwango kidogo imeng’oa nanga nchini Iran ikielekea Urusi, katika hatua ya Iran kutekeleza makubaliano kuhusu mpango wake wa nyuklia ambayo yalifikiwa tarehe 14 Julai baina yake na mataifa yenye nguvu duniani.

Hayo yamethibitishwa na Marekani. Huku kipengele muhimu cha makubaliano hayo kinaitaka Iran kupunguza akiba yake ya madini ya Urani yaliyorutubishwa kiasi hadi chini ya kilo 300.

Yakirutubishwa zaidi, madini hayo yanaweza kutumiwa kuunda silaha za nyuklia, azma ambayo nchi za magharibi zimekuwa zikiishuku Iran kuwa nayo.

 

 

Comments are closed.