MELI YA IRAN YATEKWA NYARA SOMALIA

MELI YA IRAN YATEKWA NYARA SOMALIA

Like
277
0
Tuesday, 24 November 2015
Global News

MAHARAMIA wa Somalia wameiteka nyara meli moja ya Iran iliyokuwa na wafanyi kazi 15.

Taarifa iliyotolewa na maafisa wakuu wa Somalia imeeleza kuwa Meli hiyo imetekwa nyara licha ya tahadhari iliyotolewa awali kuwa kuna uwezekano wa maharamia kuanza tena shughuli za kiharifu katika maeneo ya bahari ya Hindi.

Hata hivyo imeelezwa kwamba ingawa matukio ya uharamia yamejitokeza kwenye maeneo ya bahari hiyo karibu na ufuo wa Somalia, imebainika kuwa vitendo hivyo vimepungua kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Comments are closed.