MELI YA JESHI LA LIBYA YASHAMBULIWA 13 WAUAWA

MELI YA JESHI LA LIBYA YASHAMBULIWA 13 WAUAWA

Like
402
0
Tuesday, 04 November 2014
Global News

MELI ya Jeshi la Libya imeshambuliwa na watu 13 wameuawa katika mapigano makali yaliyoshirikisha ndege na vifaru kati ya jeshi na wanamgambo wenye itikadi kali karibu na mji wa Benghazi.

Jeshi la serikali likiungwa mkono na vikosi vitiifu kwa jenerali wa zamani, Halifa Khaftar lilifanya mashambulizi dhidi ya wanamgambo hao.

Wakaazi wa eneo hilo wamesema, raia kadhaa wanauhama mji huo,wakiitika wito wa jeshi kuwataka waondoka katika mji huo wa bandari ambako maafisa wa usalama wamesema wanamgambo wa wamejificha baada ya zaidi ya wiki mbili za mapigano.

Mwandishi  wa shirika la habari la reuters anasema ameshuhudia jeshi likiweka vifaru na silaha nzito katika mji huo wa pili kwa ukubwa nchini Libya.

 

Comments are closed.