MENEJA WA KASEJA AMFUNGUKIA MAXIMO, KAGERA SUGA YAANZA TAMBO DHIDI YA YANGA

MENEJA WA KASEJA AMFUNGUKIA MAXIMO, KAGERA SUGA YAANZA TAMBO DHIDI YA YANGA

Like
451
0
Thursday, 30 October 2014
Slider

Wakati kikosi cha Yanga kikiendelea na mazoezi huko Kahama ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Kagera sugar, uongozi wa Yanga umepewa masharti magumu kuhusu mlinda mlango wao Juma kaseja anaeonekana kusugua benchi kila kukicha ndani ya Klabu hiyo

Akizungumza na E.sports, meneja wa Kaseja, Abdulfatah Saleh, amesema haoni sababu ya kocha Maxio Maximo kuendelea kumkalisha benchi mchezaji huyo mwenye sifa kuubwa hapa nchini

Kikosi cha watengeneza sukari – Kagera sugar cha mjini Bukoba kimetoa tahadhari kwa vijana wa kocha maxio Maximo wasiingie kichwakichwa katika mchezo wao utakaopigwa siku ya jumamosi katika dimba la Kaitaba huiko Bukoba.

kocha msaidizi wa Kagera sugar Mrange Kabange amesema Yanga wanatakiwa wajue kuwa wao Kagera wamechoshwa na sare mbili mfululizo katika uwanja wa nyumbani na badala yake wanazitaka kwa udi na uvumba pointi 3 toka kwao

Comments are closed.