MEXICO imekuwa nchi ya kwanza duniani kuruhusu matumizi ya chanjo ya kukinga maradhi ya homa ya denge yanayowasibu karibu watu Milioni mia moja kila mwaka duniani, na hasa katika nchi za joto.
Idara kuu ya tiba nchini Mexico imesema chanjo hiyo ilifanyiwa majaribio kwa wagonjwa zaidi yaelfu 40,000 katika sehemu mbalimbali za dunia.
Virusi vya homa ya denge husababisha mvujo wa damu wa ndani kwa ndani na kushindwa kwa viungo kufanya kazi. Virusi hivyo vinaenezwa na mbu.