MFALME WA JORDAN AMEAHIDI MAPAMBANO YASIYO NA HURUMA DHIDI YA IS

MFALME WA JORDAN AMEAHIDI MAPAMBANO YASIYO NA HURUMA DHIDI YA IS

Like
288
0
Thursday, 05 February 2015
Global News

MFALME wa Jordan ameahidi mapambano yasiyo na huruma dhidi ya wapiganaji wa Islamic State kufuatia kuuawa kwa rubani wa nchi hiyo.

Baada ya mkutano wa makamanda wa juu wa jeshi na maafisa usalama, Mfalme Abdullah amesema vita hivyo vitaelekezwa dhidi ya kundi hilo na damu ya rubani huyo wa ndege za kivita Muath al-Kasasbeh haitapotea bure.

Hapo jana, Jordan iliwanyonga wafungwa wawili wapiganaji wenye msimamo mkali waliokuwa katika orodha ya adhabu ya kifo, kama kulipiza kisasi cha kuuawa kwa rubani wake huyo.

Comments are closed.