MFANYAKAZI WA UN ALIEAMBUKIZWA EBOLA AFARIKI UJERUMANI

MFANYAKAZI WA UN ALIEAMBUKIZWA EBOLA AFARIKI UJERUMANI

Like
322
0
Tuesday, 14 October 2014
Global News

Madaktari katika hospitali ya Leipzig wamesema mtu huyo mwenye umri wa miaka 56, alifariki dunia mapema Jumanne asubuhi.

Mlipuko huo umeua zaidi ya watu 4,000 tangu mwezi Marchi, mwaka huu hususan katika nchi za Liberia, Sierra Leone, Guinea na Nigeria.

Shirika la Afya Duniani limeuelezea ugonjwa huo kama tatizo la dharura la kiafya kuwahi kuonekana katika maisha ya sasa ya binadamu. Marekani na Uingereza ni miongoni mwa nchi zilizoanzisha utaratibu wa upimaji afya za abiria kuhusiana na ugonjwa wa Ebola katika viwanja vya ndege.

Mtu huyo alikuwa akifanyakazi kama afisa wa afya wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia- moja ya nchi zilizoathirika zaidi na maambukizi ya ugonjwa huo Afrika Magharibi- wakati alipoambukizwa Ebola.

Upimaji wa hali ya joto mwilini

Aliwasili Ujerumani Alhamisi iliyopita kwa ajili ya matibabu na aliwekwa katika kitengo maalum cha uangalizi.

“Licha ya matibabu ya kina na jitihada za hali ya juu za madaktari katika kumhudumia mwaajiriwa huyo wa Umoja wa Mataifa, hawakuweza kunusuru maisha yake kutokana na maambukizo makubwa”. Imesema taarifa kutoka hospitali ya St Georg.

Wafanyakazi wa Afya wako katika hatari kubwa ya maambukizo.

Comments are closed.