MFARANSA AUAWA KIZUIZINI MISRI

MFARANSA AUAWA KIZUIZINI MISRI

Like
322
0
Monday, 16 May 2016
Global News

Mahakama nchini Misri imewahukumu kwenda jela watu sita kwa tuhuma za kumpiga hadi kumuua raia wa Ufaransa katika kituo cha Polisi walikokuwa wamewekwa kizuizini.

Eric Lang mwenye umri wa miaka 49 aliyekuwa mwalimu wa lugha aliwekwa kizuizini nchini Misri miaka mitatu iliyopita.

Kwa mjibu wa upande wa mashitaka ni kwamba Lang aligombana na wenzake wakiwa rumande ambapo walianza kumshambulia hadi kumsababishia kifo chake.

Hata hivyo Polisi wa Misri wamekuwa wakituhumiwa kuhusiaka na mauaji ya mwanafunzi raia wa Italia Giulio Regeni aliyetoweka katika mazingira ya kutatanisha mwezi Januari mwaka huu.

Comments are closed.