Mganga aliyedai kuwa na nguvu za kuzuia risasi apigwa risasi na kufariki Nigeria

Mganga aliyedai kuwa na nguvu za kuzuia risasi apigwa risasi na kufariki Nigeria

1
718
0
Friday, 06 July 2018
Global News

Mganga mmoja nchini Nigeria amefariki baada ya mteja wake kujaribu iwapo
ana nguvu za kuzuia risasi kuingia mwilini mwake kama alivyodai.
Chinaka Adoezuwe , 26, aliuawa baada ya kumuagiza mteja wake kumpiga
risasi alipokuwa akivaa nguvu hizo za kuzuia risasi katika shingo yake.
Maafisa wa polisi katika jimbo lililopo kusini mashariki la Imo wanasema
kuwa mteja huyo sasa amekamatwa kwa madai ya mauaji
Nguvu za uganga ni maarufu nchini Nigeria , ambapo waganga huombwa
kuwatibu raia magonjwa tofauti.
Lakini kumekuwa na ripoti kadhaa za watu kula nguvu za kuzuia risasi na
dawa.
Kijana mmoja alikuwa amemtembelea mganga huyo ili kupata nguvu za
kuzuia risasi ambazo mganga huyo alimpatia, kulingana na mwanakijiji
mmoja aliezungumza na gazeti la Punch.
Ili kuthibitisha kwamba nguvu hizo zinafanya kazi , alisimama na kumpatia
mteja wake bunduki. Na hapo ndiposa janga likatokea!.
Mnamo mwezi Januari , muuzaji wa dawa za kienyeji alikamatwa baada ya
mtu mmoja aliyedaiwa kunywa maji ya kuzuia risasi kuuawa.
Muuzaji huyo anayeishi kaskazini magharibi mwa Nigeria aliripotiwa
kumhakikishia mtu huyo kwamba hatofariki atakapopigwa risasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *