MGOGORO WA SYRIA: BAN KI-MOON ATOA WAITO KUWEKA KANDO MISIMAMO MIKALI

MGOGORO WA SYRIA: BAN KI-MOON ATOA WAITO KUWEKA KANDO MISIMAMO MIKALI

Like
238
0
Friday, 30 October 2015
Global News

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa mataifa kuweka kando misimamo mikali wakati wa mashauriano mjini Vienna kuhusu mapigano yanayoendelea nchini Syria.

Aidha amewataka washiriki watano wakuu ambao ni Marekani, Urusi, Iran, Saudi Arabia na Uturuki, kuacha mtazamo wa utaifa na kukumbatia mtazamo wa kutoa uongozi kwa ulimwengu.

Hata hivyo Marekani na washirika wake wamesisitiza kwamba Rais Assad hawezi kuwa sehemu ya suluhu juu ya mzozo unaoendelea katika Taifa lake.

Comments are closed.