MH370: MATUMAINI YA KUPATIKANA KWA MABAKI ZAIDI YAANZA KUONEKANA

MH370: MATUMAINI YA KUPATIKANA KWA MABAKI ZAIDI YAANZA KUONEKANA

Like
171
0
Thursday, 06 August 2015
Global News

WAZIRI MKUU wa Australia Tony Abbott amesema kuwa ile sintofahamu juu ya ndege ya MH 370 iliyopotea inakaribia kupatiwa ufumbuzi baada ya Malaysia kutangaza kuwa mabaki ya ndege yaliyopatikana kuwa ni sehemu ya mabaki ya ndege hiyo iliyopotea. Wataalamu wamethibitisha kuwa kipande cha bawa la ndege kilichokutwa katika ufukwe wa bahari ya hindi ni sehemu ya ndege iliyopotea, iliyokuwa mali ya malaysia, waziri mkuu, Najib Razak amethibitisha hilo jana, jumatano. Razak amesema kuwa, ni siku ya 515 tangu ndege ipotee, lakini hanabudi kuwaeleza watu kuwa timu ya wataalamu kutoka mataifa mbalimbali, wamethibitisha kipande kilichoonekana ni cha ndege yao na kuongeza uhakika kuwa ndege hiyo ilianguka huko kusini mwa bahari ya hindi.

Comments are closed.