MHANDISI MANISPAA YA ILALA NA WASAIDIZI WAKE WATUMBULIWA

MHANDISI MANISPAA YA ILALA NA WASAIDIZI WAKE WATUMBULIWA

Like
284
0
Thursday, 21 April 2016
Local News

MANISPAA ya Ilala Jijini Dar es salaam imemvua madaraka mkuu wa Idara ya ujenzi mhandisi Japhery Bwigane na wasaidizi wake wawili kwa tuhuma za kusimamia ujenzi wa barabara za manispaa hiyo kujengwa chini ya kiwango.

 

Akizungumza na waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko amewataja maofisa wengine wa idara hiyo waliosimamishwa kuwa ni Siajali Mahili na Daniel Kirigiti ambao wamehamishwa idara hiyo ili kupisha uchunguzi.

 

Kuyeko amesema baraza la madiwani limefikia uamuzi huo baada ya manispaa kujiridhisha kuwa maofisa hao wamechangia kwa kiasi kikubwa kuchangia ujenzi wa barabara mbovu za manispaa hiyo.

Comments are closed.