MIAMI OPEN: MURRAY AELEZA MATUMAINI YAKE BAADA YA KUTINGA ROBO FAINALI

MIAMI OPEN: MURRAY AELEZA MATUMAINI YAKE BAADA YA KUTINGA ROBO FAINALI

Like
257
0
Wednesday, 01 April 2015
Slider

Andy Murray amekuwa Mwingereza wa kwanza kuweka historia ya kushinda mara 500 katika mchezo wa tenis baada ya kumshinda Kevin Anderson kutoka Afrika Kusini.

Murray alishinda kwa seti 6-4 3-6 6-3 na kuwa mchezaji wa 46 kushinda mara 500 tangu kuanzishwa kwa mashindano ya wazi.

Akizungumza na kituo cha BBC Murray alisema amefurahishwa na ushindi huo alioupata huko Miami sehemu ambayo ameitumia kwa muda mrefu kwakufanya mafunzo na kujinoa kwa ajili ya michuano yake, Pia ameongeza kuwa atautumia ushindi huo kama sehemu ya motisha kusonga mbele na kushinda michuano ijayo kwani mechi hiyo si ya mwisho kwake

Kwa ushindi huo Murray amefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali kwenye mashindano ya Miami Open.

Katika orodha hiyo ya wachezaji 46, tisa tu ndio bado wanaendelea kucheza mchezo huo.

Comments are closed.