MAMLAKA ya udhibiti na usimamizi wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini (SSRA) imeiagiza mifuko yote nchini kuzingatia kanuni na sheria zinazoitaka kulipa mafao ya wastaafu kwa wakati na endapo watachelewesha malipo hayo wanapaswa kulipa fidia ili kuepusha usumbufu.
Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa fedha na rasilimali watu wa (SSRA) Mohamed Nyasama wakati akitoa elimu kwa wanafunzi wanaotegemea kumaliza chuo cha mipango ya maendeleo vijijini (IRDP) mjini Dodoma ambapo amesema wastaafu wengi wamekuwa wakilalamikia usumbufu katika kupata fedha zao hivyo wanapaswa kuwalipa fidia.