MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII IMETAKIWA KULIPA MAFAO YA WASTAAFU KWA WAKATI

MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII IMETAKIWA KULIPA MAFAO YA WASTAAFU KWA WAKATI

Like
167
0
Thursday, 03 December 2015
Local News

MAMLAKA ya udhibiti na usimamizi wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini (SSRA) imeiagiza mifuko yote  nchini kuzingatia kanuni na sheria zinazoitaka kulipa mafao ya wastaafu kwa wakati na endapo watachelewesha malipo hayo wanapaswa kulipa fidia ili kuepusha usumbufu.

 

Agizo hilo limetolewa na  Mkurugenzi wa fedha na rasilimali watu wa (SSRA) Mohamed Nyasama wakati akitoa elimu kwa wanafunzi wanaotegemea kumaliza  chuo cha mipango ya maendeleo vijijini (IRDP) mjini Dodoma ambapo amesema  wastaafu wengi wamekuwa wakilalamikia usumbufu katika kupata fedha zao hivyo wanapaswa kuwalipa fidia.

Comments are closed.