MIILI YA WATU WALIOFARIKI BAADA YA KUPIGWA NA RADI YAAGWA LEO KIGOMA

MIILI YA WATU WALIOFARIKI BAADA YA KUPIGWA NA RADI YAAGWA LEO KIGOMA

Like
288
0
Wednesday, 15 April 2015
Local News

MIILI ya watu nane wakiwemo wanafunzi sita wa shule ya msingi Kibirizi, Manispaa ya Kigoma, Ujiji, Mwalimu mmoja na Mkazi mmoja wa eneo la Bangwe, waliofariki jana baada ya kupigwa na radi imeagwa leo mchana katika Viwanja vya shule hiyo ya Kibirizi.

Pamoja na Viongozi na wananchi, Shughuli hiyo pia imehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu Issa Machibya ambaye ametumia nafasi hiyo kutoa salamu zake za rambirambi kwa wanakigoma, pamoja na familia zilizopoteza wapendwa wao.

 

Comments are closed.