MAJADILIANO kuhusiana na hatua zinazoweza kuchukuliwa kimataifa kupambana na mabadiliko ya tabia nchi yamelalamikiwa kuwa yanaendelea kwa kasi ndogo .
Mazungumzo hayo yanayofanyika mjini Bonn yana lengo la kupata msimamo wa pamoja kabla ya mkutano wa mwezi Desemba wa Umoja wa Mataifa mjini Paris wakati viongozi wa dunia wataamua kuhusu makubaliano yatakayofuatwa kisheria na kila taifa duniani kote.
Kundi la mataifa yanayojulikana kama G77, chini ya uenyekiti wa Afrika kusini na kuungwa mkono na China , yamelalamika kwamba mataifa tajiri yanaonekana kuzuwia hatua za maendeleo.