MIJADALA YA HATUA ZA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI YALALAMIKIWA

MIJADALA YA HATUA ZA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI YALALAMIKIWA

Like
128
0
Thursday, 22 October 2015
Global News

MAJADILIANO  kuhusiana  na hatua  zinazoweza  kuchukuliwa kimataifa  kupambana  na  mabadiliko  ya  tabia  nchi  yamelalamikiwa kuwa yanaendelea  kwa  kasi  ndogo  .

Mazungumzo  hayo yanayofanyika  mjini  Bonn  yana lengo  la  kupata  msimamo  wa  pamoja  kabla  ya mkutano  wa  mwezi  Desemba  wa  Umoja  wa  Mataifa mjini  Paris  wakati  viongozi  wa  dunia wataamua  kuhusu makubaliano  yatakayofuatwa  kisheria na  kila  taifa duniani  kote.

Kundi  la  mataifa  yanayojulikana  kama  G77,  chini  ya uenyekiti  wa  Afrika  kusini  na  kuungwa  mkono  na China , yamelalamika  kwamba  mataifa  tajiri  yanaonekana kuzuwia   hatua  za  maendeleo.

Comments are closed.