MILIONI 568 ZATUMIKA KUJENGA VYUMBA VYA MAABARA KATIKA SHULE 17 MPANDA

MILIONI 568 ZATUMIKA KUJENGA VYUMBA VYA MAABARA KATIKA SHULE 17 MPANDA

Like
392
0
Wednesday, 19 November 2014
Local News

HALMASHAURI ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imefanikiwa kujenga vyumba 17 vya maabara kwa shule zake sita za Sekondari kwa gharama ya shilingi 568.6 milioni.

Hatua ya ujenzi wa maabara hizo umekuja ikiwa ni sehemu ya kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu ujenzi wa vyumba vya Maabara kwa Shule za Sekondari nchini.

Akiwasilisha  taarifa ya utekelezaji wa  ujenzi wa maabara kwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima aliyekuwa Mwenyekiti wa  Kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha wilaya , Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Estomihn Chang’ah amesema kuwa ujenzi umekamilika kwa asilimia 90 na kazi zilizobakia ni kuweka miundo mbinu ya vifaa vya maabara tu, kazi ambayo inatarajia kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu.

Comments are closed.