RIPOTI mpya ya shirika la afya duniani WHO, na shirika la kuwahudumia watoto UNICEF imesema zaidi ya maisha ya watu milioni 6 yameokolewa kutokana na ugonjwa wa malaria katika muda wa miaka 15 iliyopita.
Uingiliaji kati katika afya ya jamii barani Asia na eneo la mataifa ya kaukasus umekuwa na mafanikio makubwa katika kuudhibiti ugonjwa huo.
Asilimia 80 ya vifo vitakavyotokana na Malaria mwaka huu inatarajiwa kuwa katika mataifa ya Afrika kusini ya Jangwa la Sahara.