MILIPUKO YAUA ZAIDI YA WATU 40 NIGERIA

MILIPUKO YAUA ZAIDI YA WATU 40 NIGERIA

Like
192
0
Friday, 17 July 2015
Global News

WAFANYAKAZI wa uwokoaji Nchini Nigeria wamesema katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo katika mji wa Gombe watu arobaini wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya milipuko kutokea kwenye soko katika eneo hilo.

Mlipuko wa kwanza umetokea kwenye maegesho nje ya duka la viatu, na kufuatiwa na mlipuko mwingine muda mfupi baadae.

Mashuhuda wa tukio hilo amesema hali ni mbaya kwenye mitaa ya Gombe.

Comments are closed.