MISIKITI ILIYOFUNGWA YAFUNGULIWA MOMBASA

MISIKITI ILIYOFUNGWA YAFUNGULIWA MOMBASA

Like
280
0
Thursday, 27 November 2014
Global News

MISIKITI  minne iliofungwa na maafisa wa polisi wiki iliopita baada ya kuchukuliwa na vijana wenye itikadi kali za kiislamu hatimaye imefunguliwa.

Hatua ya kuifungua misikiti hiyo ya Minaa, Sakina, Musa na Swafaa inajiri baada ya siku mbili za mazungumzo kati ya viongozi wakuu wa kiislamu, wataalam na uongozi wa kaunti ya Mombasa.

Maelezo ya mazungumzo hayo yalioandaliwa na Gavana wa Mombasa Hassan Joho na kaunti kamishna Nelson Marwa yamefanywa kuwa siri.

Kabla ya misikiti hiyo kufunguliwa ,viongozi wa kiislamu pamoja na wataalam walilazimika kuajiri kiongozi wa dini wa kila msikiti na kubuni kamati maalum ya kusimamia misikiti hiyo ya kisauni na majengo mjini Mombasa.

 

Comments are closed.