MISRI: MAKUNDI YA WAPIGANAJI YAFANYA MASHAMBULIZI DHIDI YA MAAFISA USALAMA

MISRI: MAKUNDI YA WAPIGANAJI YAFANYA MASHAMBULIZI DHIDI YA MAAFISA USALAMA

Like
256
0
Wednesday, 01 July 2015
Global News

MAKUNDI ya wapiganaji yamefanya mashambulizi dhidi ya maafisa wa usalama nchini Misri katika Rasi ya Sinai.

Jeshi limesema makabiliano yanaendelea huku wanajeshi kadhaa na wapiganaji wakiuawa.Taarifa ya jeshi imesema vizuizi vitano vya polisi vililengwa sawa na kituo kimoja cha polisi.

Hili ndilo shambulio kubwa zaidi kufanywa na wapiganaji wa kiisilamu walioko eneo la Sinai, miaka miwili baada ya kuondolewa madarakani kwa Rais aliyeegemea mrengo wa kidini Mohamed Morsi.

 

Comments are closed.