MISRI YAFANYA MASHAMBULIZI YA ANGA DHIDI YA IS LIBYA

MISRI YAFANYA MASHAMBULIZI YA ANGA DHIDI YA IS LIBYA

Like
289
0
Monday, 16 February 2015
Global News

MISRI imefanya mashambulizi ya angani dhidi ya wanamgambo wa dola la Kiislamu nchini Libya, baada ya wanamgambo hao kutoa mkanda wa Video, ulioonyesha mauaji ya Wakristo wa madhehebu ya Koptik ambao ni raia wa Misri.

Waumini hao wameuawa kwa kukatwa vichwa walikuwa wamechukuliwa mateka na kundi hilo kwa wiki kadhaa.

Msemaji wa jeshi la Misri ametangaza mashambulizi hayo leo kupitia Radio ya Kitaifa nchini humo, tangazo lililoashiria Misri kukiri kwa mara ya kwanza hadharani kufanya operesheni ya Kijeshi katika nchi jirani ya Libya, nchi iliokumbwa na Ghasia kutoka kwa wanamgambo.

Comments are closed.