MISRI YAIDHINISHA HATUA MPYA YA KUPAMBANA NA UGAIDI

MISRI YAIDHINISHA HATUA MPYA YA KUPAMBANA NA UGAIDI

Like
174
0
Monday, 17 August 2015
Global News

RAIS Abdel Fattah al-Sisi wa Misri, ameidhinisha hatua mpya za kupambana na ugaidi, ambazo zimezua utata zenye nia ya kuimarisha uwezo wa taifa hilo kukabiliana na maasi ya waislamu wenye itikadi kali.

Wale watakaopatikana na hatia ya kubuni au kuongoza makundi ya kigaidi, watakabiliwa na adhabu ya kifo au kifungo cha miaka kumi au maisha jela.

Makundi ya kutetea haki za kibinadamu yamesema kuwa rais Abdel Fattah al-Sisi, atatumia sheria hizo mpya kuwafungia wapinzani wake na pia kuwazima waasi au kupinga uhuru wa kujieleza.

Comments are closed.