MISRI YAITAKA UN KUIDHINISHA HATUA ZA KIJESHI KIMATAIFA DHIDI YA IS NCHINI LIBYA

MISRI YAITAKA UN KUIDHINISHA HATUA ZA KIJESHI KIMATAIFA DHIDI YA IS NCHINI LIBYA

Like
173
0
Tuesday, 17 February 2015
Global News

RAIS wa misri Abdel Fatah Al-Sisi ameutaka umoja wa mataifa kuidhinisha hatua za kijeshi za kimataifa dhidi ya kundi la Islamic State nchini Libya.

Akizungumza na kituo kimoja cha radio cha Ufaransa, rais Sisi amesema kuwa watu nchini Libya wanataka hatua kali zichukuliwe ili kuleta usalama na udhabiti nchini mwao.

Wito wa rais Sisi unakuja siku moja baada ya ndege za kivita za Misri kushambulia ngome za Islamic State kulipiza kisasi kuuawa kwa wamisri wa dhehebu la Coptic nchini Libya siku ya Jumamosi.

 

Comments are closed.