MISRI YAZUIA NDEGE ZA SHIRIKA LA UINGEREZA

MISRI YAZUIA NDEGE ZA SHIRIKA LA UINGEREZA

Like
233
0
Friday, 06 November 2015
Global News

SERIKALI ya Misri imesimamisha safari za shirika la ndege la Easyjet ambalo lilikuwa limepangiwa kuwasafirisha baadhi ya Waingereza waliokwama mji wa Sharm el-Sheikh leo.

 

Ndege za shirika la Easyjet pamoja na ndege za mashirika ya Monarch, Thomson na British Airways ndizo zilizokuwa zimepangiwa kuwasafirisha Waingereza waliokuwa Sharm el-Sheikh baada ya Uingereza kusitisha safari za ndege za kuingia na kutoka katika mji huo.

 

Hatua hii imekuja  baada ya kuibuka kwa uwezekano kwamba huenda ndege ya Urusi iliyoanguka baada ya kupaa kutoka mji huo Jumamosi iliyopita ikiwa na abiria 224 ililipuliwa.

Comments are closed.