MIZENGO PINDA AZINDUA RASMI MKUTANO WA KIBIASHARA WA NCHI YA OMAN

MIZENGO PINDA AZINDUA RASMI MKUTANO WA KIBIASHARA WA NCHI YA OMAN

Like
367
0
Thursday, 15 January 2015
Local News

WAZIRI MKUU Mheshimiwa MIZENGO PINDA anazindua rasmi mkutano wa kibiashara wa Nchi ya Omani wenye lengo la kupanua wigo wa kibiashara na kuimarisha utafutaji wa masoko na uwekezaji leo, Jijini Dar esa salaam.

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Omani nchini Tanzania katika Sekta ya viwanda na biashara SAEED KIYUMI amesema kuwa mkutano huo utahudhuriwa na nchi Sita na Wataalamu wa masuala ya Biashara ambao watatoa mafunzo ya Kibiashara kwa wafanyabiashara wote nchini na Oman.

KIYUMI ametoa wito kwa wafanyabiashara nchini kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano huo kwani ndio fursa pekee itakayo wasaidia kujulikana kimataifa.

 

Comments are closed.