RAIS wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa anatarajiwa kuwa ni mmoja wa waalikwa wa Tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 5 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Mheshimiwa Mkapa ni kiongozi wa kitaifa ambaye anastahili kuhudhuria tamasha hilo ambalo linatimiza miaka 15 tangu kuasisiwa kwake.
Msama amesema Viongozi wengine waioalikwa, ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycalp Kadinali Pengo kwa lengo la kufikisha neno la Mungu kwa binaadam wote kwa sababu linashirikisha waimbaji wa ndani na nje ya Tanzania.