MKURUGENZI HALMASHAURI YA WILAYA YA ITILIMA ASIMAMISHWA KAZI

MKURUGENZI HALMASHAURI YA WILAYA YA ITILIMA ASIMAMISHWA KAZI

Like
441
0
Tuesday, 29 March 2016
Local News

MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Itilima mkoani Simiyu John Aloyce amesimamishwa kazi kwa tuhuma za kushindwa kuisimamia halmashauri hiyo na kusababisha kuwepo kwa migogoro kati ya madiwani na watendaji.

Uamuzi huo umechukuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka katika kikao cha dharura cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.

Mbali na uamuzi huo Mtaka amefuta posho zote kwa wakuu wa Idara na vitengo katika halmashauri zote zilizopo mkoani hapo wanaoingia katika vikao vya madiwani ikiwemo kamati za halmashauri

Comments are closed.