MKURUGENZI MAMLAKA YA BANDARI ASIMAMISHWA KAZI

MKURUGENZI MAMLAKA YA BANDARI ASIMAMISHWA KAZI

Like
324
0
Monday, 16 February 2015
Local News

KUFUATIA malalamiko ya utendaji mbovu katika kufuata taratibu za uzabuni kutoka kwa wadau mbalimbali wa Maendeleo, Bodi ya dharura ya Mamlaka ya Bandari nchini-TPA imesimamisha kazi Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo MADENI KIPANDE na kumteuwa AWADHI MASSAWE kushika nafasi hiyo hadi uchunguzi rasmi utakapokamilika.

Akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi baada ya kikao cha bodi hiyo Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa SAMWEL SITTA amesema uamuzi huo ni muhimu katika kusaidia kuleta maendelea ya kukua kwa uchumi wa Taifa kupitia Bandari.

Comments are closed.