MKURUGENZI WA TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA AOMBWA KUTUMBUA MAJIPU

MKURUGENZI WA TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA AOMBWA KUTUMBUA MAJIPU

Like
425
0
Wednesday, 17 February 2016
Local News

WIZARA ya Elimu Sayansi Teknolojia na Ufundi imemtaka Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wazima kuwasimamisha kazi Wakufunzi wakazi wa tatu, kwa kukiuka utaratibu wa kuchagua wanafunzi wa kidato cha kwanza kufuatia upotoshaji uliofanywa kwa makusudi wa kuwadanganya Wanafunzi kuwa wamechaguliwa katika shule ya Serikali jambo ambalo sio kweli.

 

Hatua hiyo imefikiwa kufuatia kuwepo kwa  Wakufunzi wakazi katika baadhi ya Mikoa kutangaza kuwa Wanafunzi hao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kama Wanafunzi wa chaguo la pili na badala yake kuwachagua katika  vituo  vya Taasisi ya Watu wazima ambayo wanafunzi huomba nafasi hizo kwa hiari yao.

Comments are closed.