MKUTANO MKUU KUJADILI MABADILIKO YA TABIA YA NCHI WAENDELEA PARIS

MKUTANO MKUU KUJADILI MABADILIKO YA TABIA YA NCHI WAENDELEA PARIS

Like
272
0
Friday, 11 December 2015
Global News

WAZIRI wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, amewasilisha rasimu ya mkataba mpya kwa wajumbe katika mkutano mkuu unaojadili kuhusiana na mabadiliko ya tabia nchi mjini Paris, kwa usiku wa pili wa majadiliano.

Fabius amesema kwamba lengo lao kuu ni kuhitimisha mazungumzo kwa dhima, sheria, matarajio,na makubaliano ya haki na ya kudumu mpaka kufikia leo, nakuongeza kusema kwamba wajumbe wa mkutano huo wanakaribia kufikia makubaliano ya mwisho.

Awali, mkurugenzi wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachojishughulisha na mazingira, Achim Steiner, alisema kwamba wajumbe wanajadiliana kuhusiana na masuala matatu ama manne, ikiwa ni pamoja na mgawanyiko kati ya mataifa tajiri na maskini zaidi dhidi ya fidia kwa kuongezeka joto duniani lilikuwa ni moja ya suala ambalo bado liko mezani kwa majadiliano.

Comments are closed.