MKUTANO WA MARAIS WATANO WA KANDA YA AFRIKA MASHARIKI WAANZA LEO

MKUTANO WA MARAIS WATANO WA KANDA YA AFRIKA MASHARIKI WAANZA LEO

Like
343
0
Wednesday, 25 March 2015
Local News

MARAIS kutoka  nchi 5 za ukanda wa Afrika Mashariki wameanza mkutano wao leo wa uwekezaji (Round Table Investment Forum) unaofanyika  jijini Dar es salaam kwa siku mbili leo na kesho March 26.

Kabla ya kuaondoka nchini  Tanzania kesho, Marais hao pia watatembelea miundombinu ya reli inayotumika kusafirisha mizigo nchi za maziwa makuu kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika usafirishaji wa bidhaa mbalimbali baina ya nchi zao.

Marais hao ni pamoja na Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkurunzinza wa Burundi, Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao wanahudhuria mkutano huo wakiwa wameambatana na  jumla ya wawekezaji 350.

Comments are closed.