MKUTANO maalum wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa unaendelea mjini Geneva kujadili hali nchini Burundi.
Kabla ya mkutano huo kufanyika mjini Geneva, Uswizi, Katibu Mkuu wa umoja UN Ban Ki-moon alikuwa ameonya kuwa taifa hilo limo hatarini ya kutumbukia kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ambayo yanaweza kuathiri kanda yote.
Amesema machafuko yaliyotokea nchini Burundi siku za hivi majuzi yanatisha na kwamba atamtuma mshauri wake maalum kwenda Burundi kwa mashauriano ya dharura na serikali.