MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA UMOJA WA AFRIKA UMEANZA LEO

MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA UMOJA WA AFRIKA UMEANZA LEO

Like
244
0
Friday, 30 January 2015
Global News

MKUTANO wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika umeanza leo nchini Ethiopia ambapo viongozi wa Afrika wanatarajiwa kujadili masuala muhimu yanayolikumba bara la Afrika kwa sasa.

Baadhi ya maswala yatakayopewa kipaumbele kwenye mkutano huo ni harakati za kundi la Boko Haram nchini Nigeria, pamoja na juhudi za kupambana dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola.

Licha ya kauli mbiu ya mkutano huo wa siku mbili kuwa swala la kuwawezesha wanawake, viongozi kutoka nchi 54 wanachama wa Muungano huo watalazimika kangazia swala la migogoro ambalo limekuwa changamoto kubwa kwa bara la Afrika.

 

Comments are closed.