MKUU WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA ASIMAMISHWA KAZI

MKUU WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA ASIMAMISHWA KAZI

Like
321
0
Monday, 22 February 2016
Local News

WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora mheshimiwa Angela Kairuki amemsimamisha kazi aliyekuwa mkuu wa chuo cha utumishi wa umma Said Nassoro kutokana na kushindwa kusimamia watumishi waliopo chini yake.

Kairuki ametoa maagizo hayo leo Jijini Dar es salaam kwenye mkutano na waandishi wa Habari katika mkutano ulifanyika chuoni hapo.

Aidha amebainisha kuwa usimamizi mbovu wa bwana Nassoro umetoa mwanya kwa viongozi mbalimbali wa matawi kufanya ubadhilifu wa mali za umma.

Comments are closed.