MKUU WA MKOA KATAVI AAGIZA WANAFUNZI WALIFAULU ELIMU YA MSINGI KUJIUNGA NA SEKONDARI

MKUU WA MKOA KATAVI AAGIZA WANAFUNZI WALIFAULU ELIMU YA MSINGI KUJIUNGA NA SEKONDARI

Like
339
0
Wednesday, 18 March 2015
Local News

MKUU wa Mkoa wa Katavi Dokta IBRAHIMU MSENGI ameagiza Wanafunzi waliohitimu Elimu ya Msingi mwaka 2014 na kufaulu kwa kuchaguliwa kujiunga na Elimu ya Sekondari, waripoti katika  shule walizopangiwa.

Dokta MSENGI ametoa kauli hiyo katika Hotuba yake iliyosomwa kwa Niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Mstaafu ISSA SELEMAN NJIKU,  wakati akifungua kikao kazi cha Viongozi,Wataalamu wa Elimu Mkoani Katavi.

Mkuu huyo wa Mkoa amehimiza kukomeshwa kwa  Watoro   Mashuleni  Wanafunzi walioacha shule wasakwe, na kurudishwa shuleni ili waendelee na masomo.

Comments are closed.