MKUU WA MKOA WA PWANI ATOA SIKU 7 ZA KUTUMBUA MAJIPU

MKUU WA MKOA WA PWANI ATOA SIKU 7 ZA KUTUMBUA MAJIPU

Like
343
0
Wednesday, 27 January 2016
Local News

MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ametoa muda wa siku saba kwa watendaji wa mitaa, watendaji wa kata na  wazazi wenye watoto waliofaulu kuingia kidato cha kwanza lakini hadi sasa wameshindwa  kuwapeleka shule wanafunzi hao, kuwapeleka shule haraka watoto wanafunzi hao.

 

Mhandisi Ndikilo ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya siku moja katika halmashauri ya mji wa Kibaha  wakati akizungumza na watumishi na watendaji mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa ambapo amesema kuwa mzazi ambaye atakaidi agizo hilo atapelekwa katika vyombo vya dola.

Mbali na hayo ameonesha kusikitishwa  baada ya kuona baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani kuna wanafunzi wamefaulu na kupata nafasi ya kuingia kidato cha kwanza  lakini mpaka sasa bado  hawaja ripoti shuleni.

Comments are closed.