MKUU wa mkoa wa Dar es salaamu mheshimiwa PAUL MAKONDA leo amemuapisha rasmi mteule mkuu wa wilaya ya kinondoni ALY SALUM HAPI ambapo amemtaka kuhakikisha anakuwa mstari wa mbele kutimiza matakwa ya mheshimiwa rais ikiwemo kupinga ufisadi na rushwa .
Awali akizungumza mbele ya watendaji ,wakuu wa wilaya na wakuu wa ulinzi na usalama, mheshimiwa PAUL MAKONDA amesema licha ya kuwa na umri mdogo inatakiwa atumie nafasi alio aminiwa na mheshimiwa rais kutekeleza majukumu hasa kuhakikisha kunakuwepo na haki kwa wanyonge .