MKUU WA WILAYA YA KINONDONI ATEMBELEA WANANCHI BUNJU

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI ATEMBELEA WANANCHI BUNJU

Like
353
0
Thursday, 28 April 2016
Local News

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Mh. Ally Hapi leo amewatembelea wananchi maeneo ya Bunju na Mbweni waliokuwa na kero mbalimbali.
Katika eneo la Bunju Kilungule, baadhi ya wananchi nyumba zao zimezungukwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. 

Akijibu maombi ya wananchi hao, Mheshimiwa, Hapi amewaagiza mainjinia wa manispaa kuhakikisha kuwa wanafanya utaratibu wa kupata pampu kubwa ya kuvuta maji hayo, huku akiwataka wananchi kuwa wale wote waliojenga  katika eneo hatarishi ambalo ramani inaonesha kuwa ni eneo la wazi wajiandae kuondoka.

Comments are closed.