MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AUNDA TUME HURU KUCHUNGUZA UBOVU WA BARABARA

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AUNDA TUME HURU KUCHUNGUZA UBOVU WA BARABARA

Like
287
0
Monday, 13 April 2015
Local News

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni PAUL MAKONDA ameunda tume huru inayojumuisha wataalamu wa mikataba, wasanifu na wahandisi na maofisa kutoka vyombo mbalimbali vya uchunguzi  kuchunguza juu ya ubovu wa barabara za wilaya ya Kinondoni  ili kujua kama usanifu wa barabara unazingatia viwango.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa Wilaya hiyo amesema wananchi wamekuwa wakiilaumu serikali kushindwa kusimamia na kukagua miradi ya barabara hali inayosababisha ongezeko la barabara mbovu.

Makonda amebainisha kuwa Wananchi wana haki ya kuhoji juu ya miradi ya barabara iliyo chini ya Serikali kwa kuwa ndio walipakodi wenyewe hivyo wana haki ya kufahamu thamani halisi ya fedha ya kodi yao kama inalingana na gharama halisi ya miradi ya ujenzi.

Comments are closed.